Top Stories

Maneno ya Rais Samia kwa Wamachinga ‘mioto DSM’

on

“Dar es salaam mmeeonesha mfano wakati wa kupangana, nafahamu kuna Watu walikuwa wanasubiri vurugu zitokee Nchi iharibike lakini mmekuwa Waungwana mmekuwa Wazalendo mmepangana bila hayo kutokea, tulisikia maneno mawili matatu lakini Viongozi wa Wamachinga mmetusaidia hali imekuwa shwari”

“Niwape pole kwa mioto inayotokea Dar es salaam tulianza kushuhudia moto Kariakoo na juzi Karume, Timu za Serikali zinakaa kuona sababu za mioto hatua zitachukuliwa ajali hizo zisitokee tena”

“Nawashukuru wakati mnapangwa kukiwa na bomoabomoa na hamishahamisha RC Makalla akazindua kampeni ya usafi na mlishiriki nae hiyo ilinipa moyo sana”

“Kundi lenu hili Serikali inalitambua vema, katika Mipango yote ya Serikali mtazamo wetu mkubwa ni kwa kundi la Vijana ” Rais Samia akizungumza na Viongozi wa Wamachinga Dar es salaam leo

Soma na hizi

Tupia Comments