Baraza la Madiwani katika Manispaa ya Geita Mkoani humo limepitisha Bajeti ya Kiasi cha shilingi Bilioni 68. 3 kwa mwaka wa fedha wa 2024/ 2025 kwa ajili ya ujenzi mbalimbali wa miundombinu.
Akizungumza Baada ya kukamilika kwa Baraza hilo Mkurugenzi Manispaa ya Geita , Yefred Myenzi amesema kwa Bajeti iliyopita walikuwa na Makusanyo ya Bilioni 59 ikiwa na ongezeko la Asilimia 13 ambapo kipindi hiki wamedhamilia kupitisha Bajeti ya Bilioni 68 .3 kutoka na vipaumbele walivyo navyo .
” Katika bajeti iliyopita tulikuwa na makusanyo ya Bilioni 59 kimsingi ni ongezeko kama la Asilimia 13 hivi lakini maeneo makubwa ambayo tumejielekeza kwenye ukusanyaji wa Mapato kwanza tumetazama vyanzo vikuu vyetu ambavyo wote tunafahamu Geita ni ya Madini , madini yanachangia asilimia kubwa , kuna mazao kuna mifugo kuna biashara nyingi , Mkurugenzi Manispaa ya Geita, Myenzi.
Katika hatua nyingine Myenzi amesema Baraza pia limepitisha Kiasi cha shilingi Bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo kubwa na lefu ( GEDEKO TOWER ) litakalosaidia kuingiza mapato kwa manispaa ya Geita.
” Vyanzo hivi vya mapato vinatuwezesha angalau mapato ya ndani ya Manispaa ya Takribani Bilioni 21 katika bilioni 68 bilioni 21 ni mapato yanayotokana na vyanzo mbalimbali vya ndani vya Manispaa mapato haya tunayaelekeza katika maeneo mbalimbali ya vipaumbele ambayo yalikuwa na mahitaji makubwa kwa manispaa ikiwemo ujenzi wa miundombinu , ” Mkurugenzi Manispaa ya Geita, Myenzi.
Elias Ngole ni Naibu Meya katika Manispaa ya Geita amesema wao kama wawakilishi wa wananchi wamepitisha Bajeti hiyo kwa lengo la kutekeleza miradi mbalimbali ya Manispaa ya Geita na wananchi wapate kunufaika na huduma hizo.
” Tumetoka kwenye baraza la madiwani kama wawakilishi wa wananchi kwa kupitisha Bajeti yenye thamani ya Bilioni 68 .3 ikumbukwe nyuma kwa bajeti tunayoendelea nayo tulikuwa na Bajeti ya Bilioni 59 kwahiyo tunaongezeko sisi matarajio yetu ni kwamba fedha hizi sasa zinaenda kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii , Naibu Meya Manispaa ya Geita, Elias Ngole.