Michezo

Manchester United na mikakati yake ya kumtema Van Persie mwisho wa msimu..

on

pesKlabu ya Manchester united haiko katika kiwango kizuri kwenye ushindani wa klabu za ligi kuu ya England na sasa inaanza kujipanga upya kwa ajili ya msimu ujao.

Habari mpya kutoka ndani ya klabu hiyo ni kuhusu mchezaji wao Robin Van Persie imesema ipo tayari kumpa ofa ya pauni milioni 5  ili aihame klabu hiyo msimu huu.

Mkongwe huyo mwenye miaka 31 amebakiza miezi 14 ili amalize mkataba wake na klabu hiyo ambayo kwa wiki imekuwa ikimlipa 250,000.

VANPamoja na klabu hiyo kutaka kumtema vigogo wa Italy Juventus na Inter Milan ziko katika harakati za kutaka kunasa saini ya nyota huyo raia wa Uholanzi huku Man U ikiwa tayari kumlipa nusu ya mshahara huku mwingine akilipwa na klabu ambayo itakuwa tayari kumchukua.

Van Persie amekuwa akiandamwa na majeruhi kwa muda mrefu lakini ameisaidia Man U kufunga magoli 10 katika ligi kuu.

millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments