Klabu ya Real Madrid ya Hispania na Manchester United kuna kila dalili za kufikia makubaliano ya kuuziana wachezaji, kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mazungumzo na mvutano kuhusu golikipa wa Man United David de Gea kujiunga na Real Madrid ya Hispania kwani walishindwa kufikia makubaliano.
Awali kulikuwa na utata wa Man United kugoma kumuachia golikipa huyo kwani walikuwa wanataka uhamisho wa David de Gea uhusishwe na uhamisho wa Sergio Ramos kujiunga Man United kabla ya beki huyo kuamua kuongeza mkataba mpya na Klabu yake ya awali ya Real Madrid.
Ila taarifa zilizotoka August 18 zinadai kuwa klabu ya Man United imekubali yaishe na iko radhi kumuachia golikipa huyo David de Gea mwenye asili ya Hispania, pamoja na kocha wa Man United Louis van Gaal kuagiza bodi kumuuza golikipa huyo kwani akili yake ipo Real Madrid na yeye hamuhitaji katika kikosi chake.
Man United haitaki kumuachia kirahisi golikipa huyo kwani imekubali kumuuza kwa Real Madrid ila inahitaji pound milioni 28 ili iweze kumuachi golikipa huyo huku Real Madrid ikihangaika kuhakikisha mpango huo unafanikiwa kwa kuwapa golikipa wake Keylor Antonio Navas ili kupunguza ada hiyo kwani walikuwa wanamuhitaji miezi 12 iliopita wakati akiwa katika klabu ya Levante kabla hajajiunga na Real Madrid.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos