Michezo

Huyu ni mbadala wa Javier Hernandez katika klabu ya Man United…….

on

Klabu ya Manchester United bado ipo katika dakika za mwisho kutafuta mbadala wa mshambuliaji wa Mexico aliyekuwa kwa mkopo wa muda mrefu katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Javier Hernandez Chicharito, Man United ambayo August 30 ili muuza Javier Hernandez kwenda katika klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani.

031315-5-SOCCER-Anthony-Martial-OB-PI.vresize.1200.675.high.25

 Man United walimuuza Javier Hernandez kwenda Bayer Leverkusen kwa dau la pound milioni 12 hivyo wametenga dau la pound milioni 36 ilikuishawishi klabu ya Monaco ya Ufaransa kumuachia Anthony Martial ajiunge na wababe hao wa Old Trafford.

64108

Hata hivyo taarifa hizo zinakuja ikiwa ni masaa kadhaa toka Man United ipoteze mchezo kwa goli 2-1 dhidi ya Swansea CityAnthony Martial ambaye analinganishwa kiuchezaji na Thierry Henry alikuwa akiwaniwa na vilabu vya Chelsea na Tottenham Hotspur ambayo ilitoa pound milioni 19 kwa Monaco zikakataliwa, bado Man United wanasubiri majibu ya ombi lao la kumnunua nyota huyo.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments