Michezo

Staa mwingine wa Man Utd aliefunga ndoa, mwimbaji PSY, Evra, Guus Hiddink wahudhuria

on

Screen Shot 2014-07-28 at 9.32.05 PMBaada ya Jonny Evans kuuaga ubachela mapema mwaka huu, leo hii zimetoka taarifa za staa mwingine wa zamani wa Manchester United ametoka kwenye chama cha mabachela baada ya kufunga ndoa na mpenzi wa siku nyingi katika harusi iliyohudhuriwa na mastaa wengine kibao.

Ji-Sung Park ambae ni nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Korea ya Kusini amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi  Kim Min Ji jana huko Gwanjangdong nyumbani kwao Korea ya Kusini.

BtjCAbGCIAAND0G

Maharusi – Park na Kim

Park ambae aliichezea Manchester United 2005 mpaka 2012 alishasambaza picha za sherehe ya kabla ya harusi mapema mwezi huu lakini harusi rasmi imefanyika jana na kuhudhuriwa na mchezaji mwenzie wa zamani wa Man Utd Patrice Evra, pia kocha wa zamani wa Korea ya Kusini – Guus Hiddink.

Staa mwingine mkubwa aliyehudhuria sherehe hizo ni muimbaji PSY staa wa hit single ya ‘gangnam Style’ na Gentleman.

hiddink-psyJPG

PSY na kocha Guus Hiddink

Ni halali yako kupata kila kinachonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB

Tupia Comments