Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu leo June 30,2022 itaanza kusikiliza maombi ya Wabunge 19 waliovuliwa uanachama na CHADEMA wakiongozwa na Halima Mdee ya kuomba Mahakama iwape kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.
Mdee na wenzake walifungua kesi hiyo dhidi ya Baraza la Wadhamini la Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Shauri hilo litasikilizwa mbele ya Jaji Mustapha Ismail, ambaye pia aliyaondoa mapingamizi ya awali yaliyowekwa katika maombi ya msingi ya kesi hiyo pamoja na maombi madogo ya kutaka hadhi za Wabunge hao zibaki kama zilivyo mpaka kesi hiyo itakapokwisha.