Naibu waziri wa Kilimo Mh Devid Silinde amehitimisha maonyesho ya Wiki ya chakula duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Kagera.
Awali ametembelea mabanda ya washiriki wa maonyesho hayo likiwemo banda la tume ya taifa ya umwagiliaji ambao wameshiriki tangu siku ya kwanza mpaka leo kilele chake.
Aidha Mh Silinde amesema kuwa serikali wana mpango wa kujenga soko la ndizi la kisasa Mkoani Kagera ili kuwasaidia wakulima Mkoani humo kupata bei nzuri ya mazao yao.
Pia amewataka washiriki wote wa maonyesho hayo kuzingatia mambo waliyojifunza ili kuboresha uzalishaji na hivyo kuwa na uhakika wa chakula na lishe kwa jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi idara ya uendeshaji kutoka tume ya Taifa ya Umwagiliaji Salome Njau amesema kuwa maonyesho hayo yamekuwa na mafanikio makubwa kwa upande wao ambapo wameweza kuhudumia wakulima takribani mia mbili na saba (207) wakipata mbinu bora za kilimo na namna nzuri ya umwagiliaji ili waweze kulima kwa ajili ya chakula na biashara kwa ujumla.
Salome ameongeza kuwa tayari wametangaza tenda kwa ajili ya uchimbaji wa visima vinne ambavyo vitanufaisha Mkoa wa Kagera huku akisema kuwa Mkurugenzi Mkuu wa tume ya umwagiliaji ameingia makubaliano na kampuni kutoka India ambayo itawapatia vifaa vya uchimbaji visima vyote Nchi nzima.