AyoTV

Miaka 38 kitandani, mke wa staa wa soka hajakata tamaa na mumewe

on

Jean-Pierre Adam ni mwanasoka wa zamani wa club za Nice na PSG alizaliwa mwaka 1948 Dakar Senegal wakati huo ikijulikana kama French West Afrika ambao ni mjumuisho wa nchi zilizokuwa makoloni ya Ufaransa (Mauritania, Senegal, French Sudan{Mali} Guinea, Ivory Coast, Upper Volta {Burkinafaso} Dahomey {Benin}).

Jean-Pierre alikuwa mwanasoka mahiri kiasi cha kupata nafasi ya kucheza timu ya taifa ya Ufaransa, ikumbukwe zamani ilikuwa ni rahisi nchi yako ikiwa koloni la Ufaransa baadhi yao walikuwa wanapata uraia wa Ufaransa kirahisi, hadi leo Ufaransa ni miongoni mwa mataifa ya Ulaya yaliosheheni raia wengi wenye asili ya watu weusi (Afrika).

March 17 1982 ulikuwa ni mwaka uliobadili mfumo mzima wa maisha ya Jean Pierre Adam na hapo ndio kuwa mwisho wa soka lake baada ya kuumia goti na kulazimika kufanyiwa matibabu kwa njia ya upasuaji, wakati ambao alikuwa na umri wa miaka 34, kabla ya kuanza kumfanyia upasuaji timu ya madaktari ilifanya makosa na kuzidisha dawa ya usingizi na kumfanya kuwa katika coma hadi leo hii hajawahi kuamka.

Kwa miaka 38 Jean-Pierre Adam hajawahi kuamka tena akiwa na umri wa miaka 72 sasa, mtu shujaa zaidi na anayetazamwa na kupewa pongezi ni mkewe Bi Bernadette Adams aliyefunga nae ndoa April 1969 ambaye amekuwa akimuangalia na kumuuguza kwa miaka yote hiyo ndani ya nyumba yao, anapika, anamsafisha na wakati mwingine humtoa na kumpeleka kwenye sofa, Jean yuko hai na anapumua pasipo kuwa na usaidizi wa kifaa chochote.

Mkewe Bi Bernadette anaamini iko siku ataamka na kuweza kuongea tena, ombi lake kubwa hatamani kuona akianza kufa yeye kabla ya Jean kwa hofu ni nani atamsaidia, wengi wanampongeza mwanamke huyo na kusema Jean-Pieere kweli hakukosea kumuoa mwanamke huyo ambaye walizaa nae watoto wawili wakiume Laurent aliyezaliwa 1969 na Frédéric aliyezaliwa 1976.

AUDIO: CORONA YAENDELEA KUMSUMBUA DYBALA WIKI YA SITA SASA

Soma na hizi

Tupia Comments