Top Stories

Mapigano DSM, kauli ya IGP “Askari wawili wamefariki, nae kauawa” (Video+)

on

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Sirro amethibitisha kuuwawa kwa Askari Polisi wawili Jijini Dar es salaam leo, Askari hao wameuwawa na mtu aliyekuwa akifyetua ovyo risasi karibu na Ubalozi wa Ufaransa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akizungumza kuhusiana na tukio hilo amesema…”Askari wetu wamefariki na huyo Bwana amefariki, kwahiyo tunafatilia kujua namna gani lakini challenge tuliyonayo ni kwamba kama mnavyojua kule Msumbiji kuna shida”

“Majeshi yetu yapo kule, ni swala la kujipanga, tumepoteza Askari wetu wawili lakini huyu Bwana aliyefanya mauaji hayo tunataka kujua ametoka wapi na ni nani halafu baadae nitawapa taarifa” –IGP Simon Sirro.

TAZAMA JAMAA ALIVYOFYATUA OVYO RISASI HEWANI HUKU AKITEMBEA BARABARANI DSM

VIDEO: POLISI WALIVYOFANIKIWA KUMDHIBITI MTU MMOJA AYELIKUWA ANAFYATUA OVYO RISASI DSM

VIDEO:ASKARI ALIVYOPAMBANA NA MTU MMOJA ALIEKUWA AKIFYATUA RISASI OVYO DSM

Soma na hizi

Tupia Comments