Shule ya First Years Academy leo imetangaza habari njema kwa Watanzania baada ya kutanua wigo wa utoaji elimu yake ya kiwango cha juu.
First Years ambao awali walikuwa na Pre Primary na Primary sasa wameanzisha rasmi shule mpya ya Secondary ya kisasa ambayo itachukua Wanafunzi 100 tu lengo likiwa ni kutoa elimu bora.
Shule hiyo ya Secondary imezinduliwa na Mkurugenzi wa Shule hiyo Mr Zoheb Bora na uzinduzi huo kuhudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo Waandishi wa habari.