Kutoka Airport Dar es salaam leo hivi ndivyo Waziri Mkuu Kasssim Majaliwa alivyowasili kwa ajili ya mapokezi ya ndege ya kwanza ya mizigo aina ya Boeing 767 -300F June 03,2023 itakayokwenda kutatua changamoto za usafirishaji wa mizigo kwa Wafanyabiashara nchini kwa kusafirisha kwa gharama nafuu na kwa urahisi, mapokezi hayo yanaongozwa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Itakumbukwa akiongea na Waandishi wa Habari juzi Jijini Dar es Salaam, Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa alisema kukosekana kwa ndege ya mizigo toka nchini kwenda Nchi za nje kumechangia ucheleweshwaji wa bidhaa pamoja na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji.
“Zaidi ya Tani elfu 24 za bidhaa ya samaki, mbogamboga na maua toka nchini zimekuwa zikisafirishwa kwa mwaka kupitia viwanja vya ndege vya nje ya Tanzania lakini ujio wa ndege hii utatoa fursa kwa Wafanyabiashara wakubwa na wadogo kusafirisha mizigo kwa gharama nafuu na kwa urahisi”
Waziri Mbarawa alisema Serikali iliamua kununua ndege hiyo kwa kuzingatia unafuu wake wa matumizi ya mafuta na kusema ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kufanya safari kwa saa kumi bila kutua kiwanja chochote.