Marekani imeshikilia taarifa kuwa ina taarifa za kijasusi zinazothibitisha kuwa Islamic State ndio waliohusika na shambulio hilo, kama walivyodai.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia alisema kuwa vyombo vyake vya usalama vina taarifa za kijasusi zinazoelekeza kwa “taasisi ya IS” kuhusika na shambulio hilo.
Msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa Adrienne Watson alisema kuwa mapema mwezi huu, serikali ya Marekani ilishiriki taarifa za kijasusi kuhusu shambulio lililopangwa kufanyika mjini Moscow.
Ujasusi huo uliufanya ubalozi wa Marekani mjini Moscow kutoa onyo kwamba “watu wenye itikadi kali” walikuwa na mipango ya kushambulia Moscow, alisema, kulingana na Reuters.
Katika tahadhari ya usalama iliyotolewa kwenye tovuti ya ubalozi mnamo Machi 7, Merika ilisema: “Ubalozi unafuatilia ripoti kwamba watu wenye msimamo mkali wana mipango ya kulenga mikusanyiko mikubwa huko Moscow, kujumuisha matamasha, na raia wa Amerika wanapaswa kushauriwa kuepuka mikusanyiko mikubwa. saa 48 zijazo.”