Shirika la Kulinda Mazingira la Marekani (EPA) lilipendekeza Jumatano, Aprili 12 kupunguza kwa kiasi kikubwa hewa chafu kutoka kwa magari mapya. Lengo ni kupunguza wastani wa uchafuzi wa mazingira kwa 13%. Ni pendekezo linalohitajika zaidi hadi sasa nchini Marekani.
Ili kufikia hili, makampuni ya kutengeneza magari yanapaswa kinadharia kuzalisha 67% ya magari ya umeme ifikapo mwaka 2032 na takwimu muhimu wakati 6% pekee ya magari ya Marekani yaliyouzwa mwaka jana yalikuwa ya umeme.
Utawala wa Marekani unataka kupunguza hatua kwa hatua kiasi cha hewa chafuzi inayozalishwa na inabakia kwa makampuni ya kutengeneza
Magari na kuchagua kati ya teknolojia kadhaa: kupunguza magari yao, kuboresha injini zao au hata kubadilisha vichujio vya chembe.I
kiwa sheria mpya zitazingatiwa, uzalishaji wa CO2 unaweza kupunguzwa kwa karibu tani bilioni 10 hadi mwaka 2055 huku upande wa wanamazingira wanasema, hii pia itapunguza gharama za mafuta na uagizaji wa mafuta.
Hata hivyo, matatizo kadhaa yanaonekana kuwa kwa kiasi kilichopunguzwa cha malighafi inayopatikana kama vile lithiamu au idadi ndogo ya vituo vya kuchaji lakini pia viwango vinavyoweza kubadilika kwa kila mabadiliko ya kisiasa Jambo ambalo hufanya iwe vigumu kwa makampuni kujipanga kwa muda mrefu.
Ongezeko la mkusanyiko wa magari huchangia mno kwenye uchafuzi wa hewa na mabadiliko ya tabianchi; kote ulimwenguni, sekta ya uchukuzi huchangia takribani robo ya uzalishaji wa gesi chafu inayosiana na gesi ya ukaa. Hasa, uzalishaji wa gesi kutoka kwa magari ndicho chanzo kikuu cha chembechembe laini za (PM2.5) na nitrojeni oksidi (NOx) ambazo ni chanzo kikuu cha uchafuzi mijini.