Habari za Mastaa

Baada ya miaka kumi na nne ya kazi, Guiliana Rancic atangaza kuondoka E!News…!!

on

GR4

Kama wewe ni mfuatiliaji wa stori za mastaa wa Hollywood basi utakuwa unakifahamu vizuri kipindi cha E!News kinachorushwa na kituo kikubwa cha burudani Marekani E!Entertainment na bila shaka utakuwa unamfahamu vizuri mtangazaji wa kipidi hicho Guiliana Rancic.

GR5

Guiliana Rancic mtangazaji wa E!News

Headlines kutoka Marekani leo zinamhusu entertainment personality na Tv presenter Guilana Rancic, ambae baada ya miaka 14 ya kufanya kazi na E!Entertainment ametangaza kuacha kazi na kituo hicho cha Tv.

gr9

Kumekuwa na maneno mengi kuhusiana na yeye kuacha kazi, Guiliana ameamua kuongea na kuweka wazi sababu zilizomsukuma kuacha kazi E!News, kwenye interview moja aliofanya Guiliana alikuwa na haya ya kusema:

gr10

>>>“Maamuzi ya mimi kuacha kazi ni maamuzi niliyoyafanya mwenyewe kwa asilimia mia, haya sio maamuzi ya ghafla, nimekuwa nikitaka kuondoka E!News muda mrefu toka miaka mitatu iliyopita lakini E!News wamekuwa wakipeleka tarehe mbele”. <<< Guiliana Rancic.

GR2

>>> “Nimefanya kazi na E!News kwa miaka 14 na safari yangu imekuwa nzuri iliyonifundisha mengi kwani walinipokea nikiwa bado mdogo nisiyejua vitu vingi kwenye hii industry, lakini baada ya miaka 14 nahisi wakati umefika wa mimi kujaribu vitu vingine kama mfanyabiashara na entertainment personality, ila bado nitakuwa na-host red carpet events za E!Entertainment”. <<< Guiliana Rancic.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments