Premier Bet SwahiliFlix Ad Tigo Ad

Habari za Mastaa

Bunduki za AK47 na wanajeshi kwenye msiba wa baba yake Jidenna Nigeria?! (Audio)

on

JIDENNA

Jidenna ni msanii kutoka Wisconsins Marekani aliyechini ya Wondaland Records inayosimamiwa na Janelle Monae.

Jidenna amefahamika zaidi na single yake ya Classic Man na kama ulikuwa hujui msanii huyu ana asili ya Kiafrika  mama yake akiwa mzungu na baba yake Mnigeria na jina lake ni la kiluga na lina maanisha “kumkumbatia baba”.

JIDENNA JANELLE

Jidenna na Janelle Monae kwenye picha ya pamoja.

Nimekutana na interview moja aliofanya msanii huyu na swali kubwa kwake lilikuwa ni changamoto gani anazozipata Marekani akiwa ni mtu mwenye mchanganyiko wa Kiafrika na sio Mmarekani mweusi.

Jidenna alikuwa na mengi ya kusema, lakini kikubwa kilikuwa kuhusu msiba wa baba yake ambao anasema ilimbidi aende na bunduki za AK47  na kundi la wanajeshi kwa ajili ya ulinzi wa familia yake…

HOLLYWOOD, CA - MAY 13:  Jidenna performs onstage during "American Idol" XIV Grand Finale at Dolby Theatre on May 13, 2015 in Hollywood, California.  (Photo by Kevork Djansezian/Getty Images)

>>>“Ukiwa mchanganyiko wa mzungu na mweusi kwa kule kwetu unashambuliwa na kila mtu, kwa mfano tulivyoenda kijijini kwetu Nigeria kumzika baba yetu ilitubidi twende na bunduki nyingi za AK47 na tulikodi kikundi cha wanajeshi kwa ajili ya ulinzi wetu … “ <<< Jidenna

www

Jidenna kwenye pozi la picha na mmoja ya mashabiki.

>>>“ukiwa shombe kijjini kwetu unaonekana una hela, una thamani, wewe mzungu, wewe Mmarekani kwahiyo kutekwa ni rahisi sana, kabla ya kuja huku tulipata sana shida Nigeria, tulikuwa tunavamiwa mara kwa mara, lakini tulivyokuja Marekani hali ilikuwa tofauti kabisa…” <<< Jidenna.

Nimekusogezea kipande cha interview akiwa anaelezea hali hiyo hapa chini.

 Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments