Mix

Hii hapa taarifa ya Marekani ikiituhumu Sudan kushambulia raia wake.

on

sudan

Marekani imeituhumu Sudan kwa kufanya mashambulio dhidi ya raia wake katika majimbo ya Kordofan kusini na Blue Nile .

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa , Samantha Power amelaani mashambulio hayo ambayo alisema yalilenga shule na hospitali.

Bi Power amesema kuwa tangu mwezi April mamia ya makombora yamekuwa yakirushwa kwa ndege za kijeshi za Sudan katika miji na vijiji katika kanda hiyo .

power

Zaidi ya watu milioni wameripotiwa kuyakimbia makazi yao kutokana na mashambulizi hayo.

Mapema mwanzoni mwa wiki, mashirika ya misaada yaliliandikia baraza la usalama la umoja wa mataifa, umoja wa Afrika pamoja na jumuiya ya nchi za kiarabu yakitaka mashambulizi dhidi ya raiya yasitishwe na serikali ya Sudan.

Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.

Tupia Comments