Michezo

Mariga akubali kushindwa Ubunge Kenya

on

Mchezaji wa zamani wa club za Inter Milan na Parma za Italia McDonald Mariga ameamua kupiga simu na kumpongeza mshindani wake Imran Okoth katika jimbo la Kibra kutoka chama cha ODM.

McDonald Mariga alikuwa anagombea Ubunge wa jimbo la Kibra November 7 2019 kupitia chama cha Jubilee na Imran Okoth alikuwa anagombea nafasi hiyo kupitia chama cha ODM na kufanikiwa kuibuka mshindi kitu ambacho kimemfanua Mariga ampigie simu na kumpongeza.

“Hello Mimi ni Mariga nimekupigia kukupongeza ushindani ulikuwa ni mzuri, nakuahidi kufanya kazi na wewe na tunaweza kukutana kwa ajili ya chakula cha mchana na ukitaka sapoti yoyote kutoka kwangu, hata baada ya huu uchaguzi tunaweza kuendeleza urafiki wetu”>>> McDonald Mariga

Katika uchaguzi huo mdogo wa kuziba nafasi ya ubunge wa jimbo la Kibra baada ya kuwa wazi kutokana na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kufariki, Imran Okoth alikuwa anaongoza kwa kwa takribani 60% ya kura na Mariga kuona kama hawezi kushinda amkampigia kumpongeza kabla ya matokeo ya jumla kutangazwa.

VIDEO: BAADA YA KUFUKUZWA AYO TV IMEMFUATA ZAHERA KWAKE “SIJAPEWA BARUA”

Soma na hizi

Tupia Comments