Michezo

Ujumbe wa Mario Balotelli kuhusu Euro 2016 unaoshangaza wengi !!!

on

Kuelekea michuano ya Euro 2016 mshambuliaji wa Liverpool aliyepo kwa mkopo katika klabu ya AC Milan ya Italia Mario Balotelli, ameingia katika headlines baada ya kuandika ujumbe ambao hadi sasa unashindwa kueleweka kuwa staa huyo amekusudia nini au lengo lake hasa ni nini?

Mario Balotelli ameingia katika headlines baada ya kuandika ujumbe katika account yake ya Instagram unaohusiana na michuano ya Euro 2016 inayotegemea kufanyika Ufaransa, Balotelli ambaye amepoteza namba katika kikosi cha timu ya taifa ya Italia aliandika ” Can’t wait” huku akiambatanisha na picha ya kundi B ambalo lina timu za Ubelgiji, Ireland, Sweden na Italia.

23

Kinachoshangaza ni kuwa Balotelli kamaanisha nini? kuwa ana hamu ya michuano hiyo kucheza au kuangalia kwenye TV timu yake ya taifa ikicheza? kwani kama ni kucheza hana uhakika wa kuitwa katika kikosi hicho kutokana na kiwango chake kudaiwa kushuka, hadi kufikia Liverpool kumtoa kwa mkopo AC Milan. Balotelli aliibuka shujaa katika michuano ya Euro 2012 baada ya kufunga goli mbili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Ujerumani na kuipeleka Italia fainali.

Hii ni video ya magoli aliyofunga Mario Balotelli Euro 2012

https://youtu.be/7NSkoPAuqpI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments