Msanii wa Bongofleva Marioo leo ametangazwa rasmi kuwa balozi wa kampuni ya michezo ya ubashiri ya Parimatch mbele ya waandishi wa habari, baada ya kutangazwa huko maswali yalikuwa mengi kutoka kwa waandishi wakitaka kujua thamani ya mkataba huo wa mwaka mmoja ambapo Marioo aliamua kufanya siri.
Marioo ambaye hili ni dili lake la pili 2022 baada ya lile la Tigo, ameeleza kuwa ameamua kuweka siri thamani mkataba wake kwa sababu kadhaa licha ya kuwa nchi kama Nigerią wasanii wanaweka wazi thamani ya mikataba yao.
Wengi wakataka kufahamu Marioo imani ya dini yake inamruhusu kuwa balozi wa kampuni za ubashiri, maana Alikiba aliwahi kusikika akisema hawezi kuwa balozi wa ubashiri.
“Masuala ya imani ya dini niachie mimi na imani yangu Mungu ndio kiła kitu naamini pia hii riziki (Dili Ła Parimatch) yeye ndio ameimwagia baraka zote mimi kuipata”>>> Marioo