Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amepiga marufuku ya upigwaji wa ngoma za vigodoro pamoja ngoma ya kanga moja maarufu kama Kanga Moko katika Mkoa huo.
Ayoub amesema kumekuwa na kawaida kwa Wananchi kutoka katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar kuja katika Mkoa wa Kaskazini na kuja kucheza ngoma na starehe.
“Sio ruhusa kwa Wakazi wa Mkoa wa Kaskazini na Wananchi wanaokuja kutoka sehemu mbalimbali kuja kupiga ngoma na kucheza vigodoro na kanga moja “kanga moko”
Ameyasema haya wakati akitoa taarifa kwa Waandishi kuhusu muelekeo wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kwenye miaka mitano ijayo Ofisini kwake Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja.