Top Stories

‘Marufuku mikusanyiko katika Wilaya ya Songwe’- DC Simalenga (Video+)

on

Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Saimon Simalenga amepiga marufuku makongamano na mikusanyiko isiyo ya lazima ndani ya Wilaya hiyo kwa lengo la kuwakinga Wananchi na maambukizi ya Virusi vya Corona. Simalenga ametoa katazo hilo jana wakati akizungumza na Wandishi wa Habari Wilayani Songwe.

Hata hivyo, Simalenga amesema marufuku hiyo haiwahusu waumini wa dini zote ambao wanaruhusiwa kuendelea kufanya ibada kama Kawaida, lakini akiwataka wachukue tahadhari dhidi ya virusi vya Corona wanapokuwa ibadani.

“Kuanzia sasa hakuna mikusanyiko isiyokuwa ya lazima itaruhusiwa kufanyika ndani ya Wilaya ya Songwe, tunazuia mikusanyiko hivyo kwa nia njema ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virus vya Corona,” alisema Simalenga.

Simalenga amesema kila atakayetaka kufanya kongamano lolote lazima awasiliane na ofisi ya Mkuu wa Wilaya kabla hajafanya ili apewe kibali kwa kuzingatia mazingira yaliyopo na kama Serikali itajiridhisha kuwa msongamano huo hautakiwa na athari za kiafya kwa Wananchi.

Tupia Comments