Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji, Angella Kairuki amezitaka taasisi za Kidini na zisizo za kidini kujitolea kuchangia damu katika Hospitali mbalimbali ili kukabiliana na upungufu wa damu.
Waziri Kairuki ameyasema hayo alipokutana na mbunge wa Temeke, Abdalla Mtolea na Mkurugenzi wa Al Hikma Sheikh Nurdin Kishki katika Hospitali ya Temeke wakati wa uchangiaji damu.
“Natoa rai kwa taasisi za kidini na nyingine mbalimbali wasisiti kuchangia damu na kufanya usafi katika mahospitali kwani kuna wagonjwa wengine wanatoka mikoani na hawana ndugu kabisa,”amesema