Top Stories

Mashabiki waingia kwenye puto Tamashani kujikinga na corona (+picha na video)

on

Bendi ya muziki wa rock ya The Flaming Lips ya Oklahoma Marekani imefanya tamasha la aina yake ambapo Mashabiki na Wanamuziki kila mmoja aliingia ndani ya puto la plastiki ikiwa ni njia mpya ya kuenjoy muziki kwenye tamasha lakini wakati huohuo kujikinga na corona.

The Flaming Lips

Tamasha hili lililofanyika Oklahoma imeelezwa ni majaribio ya ukawaida utakaokuwepo kwenye matamasha yajayo kwenye dunia ya sasa ambayo inasumbuliwa kichwa na kirusi corona.

Kwenye Tamasha hili lililofanyika Marekani ambako kuna Watu milioni 8 waliopatwa na virusi vya corona, kulikua na maputo 100 ambapo kila moja lilikua na Shabiki wa Bendi hiyo ndani ambapo Msemaji wa Bendi hiyo amesema hakuna aliefahamu kama corona ingeendelea kuwepo hadi sasa, ilionekana ni kitu cha kupita tu muda mfupi.

Idea hii ya kuweka Watu kwenye maputo kama hivi ilitambulishwa na wao kwa mara ya kwanza mwezi May 2020 ambapo Msemaji wa Bendi hiyo amesema ukiwa ndani ya hili puto unaweza kupiga kelele uwezavyo, unaweza kucheza uwezavyo lakini huwezi kumuambukiza jirani yako.

VIDEO HII HAPA CHINI…

KUTANA NA BEATRICE, MUUZA KEKI MPAMBANAJI MWENYE MASTERS 2…

Soma na hizi

Tupia Comments