Top Stories

Mashabiki wamjia juu Keita kwa kujichubua

on

Mchezaji wa timu ya taifa ya Senegal, Keita Balde awashangaza mashabiki wa soka nchini kwao kwa kubadilisha muonekano wake na kuwa mweupe tofauti na mwanzo alivyokuwa.

Keita Balde mwenye umri wa miaka 26 mchezaji wa Cagliari inayoshiriki ligi ya Seria A nchini Italia, alizaliwa nchini Spain na wazazi weusi wenye asili ya Senegal. Keita alichagua kuwakilisha taifa la Senegal walikotekea wazazi wake na kucheza mechi ya kwanza na timu ya taifa March 16, 2016.

Keita amekuwa gumzo katika michuano ya AFCON mwaka huu nchini Cameroon mashabiki wakimsema katika mitandao ya kijamii kwa kujibadilisha muonekano.

Keita yupo kwenye mahusiano na mrembo Simona Guatieri, aliyewahi kuwa mshiriki wa Miss Dunia, na Miss Italia na mpaka sasa wamefanikiwa kupata watoto wawili.

Soma na hizi

Tupia Comments