Michezo

Mashabiki wavamia nyumba ya Ed wa Man United

on

Baada ya nyumba ya makamu mwenyekiti wa Man United Ed Woodward ,48, kuvamiwa na wanaohisiwa kuwa mashabiki wa Man United wakiimba nyimbo za gadhabu na kurusha baruti kwenye nyumba ya kiongozi huyo, Man United yasema wakibainika waliofanya tukio hilo watafungiwa.

Man United wamefika mbali zaidi na kutoa onyo kuwa wanaheshimu hisia za mashabiki lakini hawawezi kuvumilia na kufumbia macho vitendo vya ovyo kama hivyo, hata hivyo wakati hayo yanatokea ED Woodward hakuwepo nyumbani kwake.

Kwa siku za hivi karibuni mashabiki wa Man United wamekuwa wakimtuhumu mtendaji huyo kuwa ni miongoni mwa wanaokwamisha mafanikio ya timu ikiwemo kutosaini bajeti ya kutosha kufanya usajili, kitu ambacho kiliwahi kumtofautisha na kocha wa Man United aliyepita.

Soma na hizi

Tupia Comments