Habari za Mastaa

Salama Jabir na Solo Thang wameyasema haya yawafikie mashabiki wa Ali Kiba na Diamond

on

SalamaUpinzani unaokuzwa na mashabiki kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba kwenye mitandao ya kijamii umepelekea Mastaa wa Tanzania kuanza kujitokeza hadharani na kuwaweka mashabiki hawa sawa kwa kuamini wamevuka mipaka kwenye ushabiki.

Mtangazaji wa TV show ya Mkasi Salama Jabir na msanii mkongwe bongoflevani Solo Thang ni miongoni mwa waliozipaza sauti zao June 30 2015.

Kupitia kwenye ukurasa wa twitter Salama Jabir aliandika ‘Wabongo tumekua wakosoaji mpaka wasanii wanajishtukia, hakuna “zuri kabisa” kwenye macho yetu… tuwaache wasanii wawe “Wasanii” nadhani!

.Jana tulikua tunaongea na wana job, Ali Kiba hakuwa mtu wa vioo vikali, yeye alikuwa anatoa audio kali na video ya Mwananchi kamaliza, zama zimebadilika mpaka anakwea pipa kwenda kutoa kideo kikaaali tushukuru, kapendeza, rangi nzuri! mengine tuyaache..’  kauli ya Salama Jabiri

.Upinzani huo ulioanzishwa na makundi yanayojiita (TeamAliKiba na TeamDiamond) yalimkwaza pia mkongwe wa Hip Hop Solo Thang na kuandika..’Ukiweka habari au picha au muziki wa msanii muyu mashabiki  wa yule wanakutukana!  kwanini? ? hii burudani tu isiwe uhasama, tujivunie sanaa yetu..’

solo 1

Solo Thang

 

TAZAMA YA VANESSA MDEE HAPA CHINI…

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments