Michezo

LaLiga: Matokeo ya Real Madrid vs Villareal na walichokifanya mashabiki wa Man United vyote viko hapa

on

1411830960089_wps_25_Real_Madrid_s_Cristiano_RBaada ya kuifumua Elche magoli 5-1 katikati mwa wiki hii, Real Madrid leo walisafiri mpaka katika dimba la EL Madrigal kukipiga dhidi ya Villareal katika mchezo wa kugombea uchampion wa ligi kuu ya Hispania – Laliga.

Wakicheza kwa kujihami Villareal waliruhusu nyavu zao kuguswa katika dakika ya 32 baada ya Luka Modric kuipatia Madrid goli la kuongoza.

Mwanasoka bora wa ulaya na dunia Cristiano Ronaldo kwa mara nyingine tena wiki hii akaifungia Madrid goli la pili katika dakika ya 40 ya mchezo huo.

Mpaka mwamuzi anapuliza kipenga Madrid walikuwa na ushindi wa 2-0 kibindoni.

1411833935717_wps_5_epa04420167_View_of_a_pla

Lakini wakati mchezo huo ukiendelea kikundi cha mashabiki wa Man UNited wanaojiita ‘United Reel’ walitimiza ahadi yao ya kurusha ndege juu ya uwanja huo huku ikiwa na ujumbe kwenye kwa Ronaldo kwamba arudi nyumbani Manchester.

Tupia Comments