Jeshi la Israel limefanya mashambulizi mapya katika eneo la Gaza na yamesababisha vifo vya watu 42 siku ya Jumatano wakati majeshi ya Israel yakizidisha mzingiro wa maeneo ya kaskazini ya eneo la Palestina, hospitali zinazozunguka na makao ya wakimbizi, na kuwaamuru wakaazi kuelekea kusini, madaktari na wakaazi walisema.
Wizara ya afya ya Gaza na Shirika la Afya Duniani walisema hawataweza kuanzisha kampeni ya chanjo ya polio kaskazini mwa Gaza kama ilivyopangwa kwa sababu ya mashambulizi makali ya mabomu, kuhama kwa watu wengi na ukosefu wa njia.
Takriban Wapalestina 42,847 wameuawa na wengine 100,544 kujeruhiwa tangu Israel ilipoanzisha vita vyake dhidi ya Gaza Oktoba 7 mwaka jana, kwa mujibu wa Wizara ya Afya katika eneo hilo.
Katika muda wa saa 24 zilizopita, mashambulizi ya Israel katika ukanda huo yaliua takriban Wapalestina 55 na kujeruhi watu 132, wizara hiyo iliripoti Alhamisi