Yale mashindano makubwa yaliyokuwa yakisubiriwa kwa muda mrefu mashindano ya magari Afrika unaofahamika kama “Afrika Rally Championship 2023 yataanza kutimua vumbi kwa siku mbili kuanzia tarehe 11/ 12 katika shamba la ASAS Matembo Iringa vijijini na Shamba la Miti la Sao Hili Iliyopo wilayani mufindi mkoani Iringa.
Kwa mara ya Kwanza mashindano haya kwa mara ya kwanza yamedhaminiwa na kampuni ya ASAS na mashindano haya yatafanyika kwa pamoja na Mashindano ya magari ya Taifa (National Rally Championship ) na uzinduzi wake umefanyika leo katika uwanja wa samora Iringa .
AYO TV imezungumza na Rais wa Chama cha mbio za magari Tanzania (AAT) Nizar Vijan ambapo amesema jumla ya madereva 17 wameshiriki mbio hizo ambapo 7 wanashiriki mbio za Afrika na 10 mbio za Kitaifa
Mkurugenzi wa kampuni ya ASAS @ahmed Asas amesema lengo la mashindano haya ni kuimarisha utalii na kufungua lango ka kiutalii kusini pamoja na upandaji wa miti pamoja na utunzaji wa mazingira