Jumatatu Novemba 20, 2023: Mashindano ya Safari Lager Cup yanayodhaminiwa na Bia ya Safari Lager, yamezidi kunoga huku timu nne zikitangazwa.
Msemaji wa mashindano hayo, yaliyoleta msisimko wa aina yake, Mbwiga Mbwiguke, alisema zoezi hilo la kuibua vipaji, liliendeshwa k iwa ukamilifu kama ilivyopangwa na tayari wachezaji 22 kutoka kila Mkoa wameshachaguliwa.
“Kama tulivyowaarifu hapo awali, zoezi hili lilishirikisha mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha na hatimaye Dar es Salaam ambapo makocha mahiri Jamhuri Kihwelo na Sekojo Chambua walikuwa na kazi ngumu ya kuchagua kikosi Cha wachezaji 22 kutokana na bonanza mbalimbali walizoshiriki baada ya usaili,”alisema.
Alisema hatua inayofuata sasa ni timu hizo nne kushindanishwa na Kisha makocha watachagua timuu moja itakayojulikana kama Safari Lager Champions ambayo hatimaye itacheza na timu mojawapo ya Ligi Kuu Tanzania.
Meneja wa Bia ya Safari Lager Pamela Kikuli, aliwapongeza makocha Jamhuri Kihwelo na Sekojo Chambua Kwa kuendesha zoezi Hilo Kwa weledi mkubwa na kutumia uzoefu wao kuchagua timu hizo.
Alisema bia ya Safari, ambayo ni ya mabingwa iliamua kuja ya kampeni hii ili kuibua vipaji vipya kabisa vya mpira wa miguu kwani wanaamini kuna vipaji vingi nchini ambavyo havijaibuliwa.
Aliongeza kuwa hatua inayofuata itakuwa na msisimko mkubwa kwani timu nne zilizochaguliwa zitachuana ili kupata timu moja ya wachezaji 22 itakayocheza na timu ya Ligi Kuu.