Mapema wiki hii, Ikulu ya Marekani ilitoa tamko kwamba mashirika yote ya kiserikali yamepewa siku 30 kuhakikisha kuwa yanasitisha matumizi ya application ya TikTok kwenye vifaa na mifumo ya shirikisho. Katika jitihada za kuhakikisha usalama wa taarifa na data za kutoka nchini Marekani, mashirika yote ya shirikisho lazima yaondoe TikTok kutoka kwenye simu na mifumo ya serikali, Mkurugenzi wa Ofisi ya Usimamizi na Bajeti Shalanda Young aliambia mashirika katika ya hati ya mwongozo iliyoonekana na shirika la Habari la Reuters.
Mtandao huo una zaidi ya watumiaji bilioni moja duniani ikiwa ni pamoja na zaidi ya watumiaji milioni 100 nchini Marekani, ambapo imekuwa nguvu ya kitamaduni, hasa miongoni mwa vijana, ambayo imezua wasiwasi miongoni mwa wabunge. Serikali ya Marekani imesema iko tayari kuchukua hatua kubwa zaidi ili kukomesha matumzi ya TikTok huku sheria za kupiga marufuku application hiyo nchini Marekani ikianza kupitiwa na Bunge la Marekani.
Nchi ya Denmark pamoja na Canada zimeongezeka kwenye orodha za nchi zilizotangaza kupiga marufuku matumizi ya Tiktok kwenye vifaa vya serikali, Bunge la Denmark likiwataka wabunge kwamba wabunge na wafanyakazi kuondoa application ya TikTok kutoka kwenye simu zao ili kuepuka athari za kijasusi, huku kitengo cha utendaji kwenye Uomoja wa Ulaya ikifanya hivyo hivyo.