Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Mashtaka mapya ya Sabaya aliyofunguliwa Moshi
Share
Notification Show More
Latest News
Huyu ndie Kizz Daniel, Bilionea wa Buga, Mikasa ya Polisi mpaka kupelekwa Mahakamani
August 12, 2022
Basi la New Force latumbukia korongoni, Mmoja afariki, Polisi anena chanzo
August 12, 2022
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 12, 2022
August 12, 2022
PICHA: Matukio ya Mkutano Mkuu wa CAF uliyofanyika Tanzania
August 11, 2022
Ndugu abiria kulipwa Milioni 150, Wakili aibua mapya ‘Watu binafsi waliopost meme wajiandae’
August 11, 2022
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > Mashtaka mapya ya Sabaya aliyofunguliwa Moshi
Top Stories

Mashtaka mapya ya Sabaya aliyofunguliwa Moshi

June 1, 2022
Share
2 Min Read
SHARE

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya leo Juni 1.2022 amefikishwa katika Mahakama ya hakimu Mkazi Moshi Mkoani Kilimanjaro akiwa na wenzake watano kwa makosa saba ya uhujumu uchumi.

Akisoma mashtaka hayo yanayomkabili Sabaya na wenzake, Mwendesha mashataka wa Serikali Tumaini Kweka amesema kuwa Sabaya na wenzake wanne Sylvester Nyegu, John Odemba Aweyo,Nathan Msuya na Antheo Boniface Assey wanashtakiwa na makosa saba ya uhujumu uchumi ikiwemo kuongoza genge la uhalifu, kutenda kinyume na mamlaka yake, kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na utakatishaji wa fedha haramu.

Hata hivyo Wakili upande wa utetezi Hellen Mahuna ameiomba Mahakama hiyo kufuata sheria ili kutenda haki akidai kuwa wateja wake na Mahakama ya Arusha haikupata kibali halali cha kuwatoa washtakiwa gereza la Kisongo Arusha na kuwapeleka gereza la Karanga Moshi.

Kwa upande wake Sabaya aliyeomba kuongea licha ya Hakimu kueleza kuwa maombi yake hayatazingatiwa kwa sasa alieleza mahakamani hapo kuwa hana imani na Mwendesha mashtaka wa serikali Tumaini Kweka.

Sabaya akiwa anatokwa na machozi mahakamani amesem hana imani na Mwendesha mashtaka wa serikali Tumaini Kweka kwa kuwa anatokea Wilaya ya Hai Kijiji cha Makoa nilipo kuwa nafanyia kazi, anatumikaa kisiasa na anachuki, nakuomba Rais Samia alione hili linalofanyika Kilimanjaro katika kesi hiyo na kwamba hao anaoshtakiwa nao wanateseka bure pamoja na yeye ikiwa Kweka ataendelea na kesi hiyo

Kufuatia mabishano hayo Hakimu Mkazi Mfawidhi aliyekuwa anasikiliza shauri hilo Salome Mshasha aliahirisha usikilizaji wake kwa muda wa dakika kumi (10) ili apate kupitia sheria juu ya yaliyotajwa huku akidai kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayo mkabili Sabaya na wenzake.

Kesi ya hiyo ya uhujumu uchumi namba 2 ya mwaka 2022 imeahirishwa hadi Juni 7,Mwaka huu na Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Moshi,Salome Mshasha.

You Might Also Like

Basi la New Force latumbukia korongoni, Mmoja afariki, Polisi anena chanzo

Ndugu abiria kulipwa Milioni 150, Wakili aibua mapya ‘Watu binafsi waliopost meme wajiandae’

Ajali Mbaya!! Watu sita wafariki, Polisi wafunguka, chanzo ‘Dereva alikuwa Mwendokasi, lilipinduka’

Hafla ya makabidhiano ya data za utafutaji wa Mafuta na Gesi asilia kwa vitalu Zanzibar

Ukumbini: Bwana Harusi aonesha video ya mkewe akiwa faragha na shemeji yake chumbani

TAGGED: TZA HABARI
Pascal Mwakyoma TZA June 1, 2022
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Maagizo ya Makamba “Vijiji vyote vipate umeme”
Next Article VideoMPYA: Mr Firewood ngom inaitwa “Leo”
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Huyu ndie Kizz Daniel, Bilionea wa Buga, Mikasa ya Polisi mpaka kupelekwa Mahakamani
Entertainment August 12, 2022
Basi la New Force latumbukia korongoni, Mmoja afariki, Polisi anena chanzo
Top Stories August 12, 2022
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 12, 2022
Magazeti August 12, 2022
PICHA: Matukio ya Mkutano Mkuu wa CAF uliyofanyika Tanzania
Sports August 11, 2022

You Might also Like

Sports

Kauli ya Simba SC baada ya Tundaman kuingia na Jeneza ‘Simba day’ uwanja wa Mkapa

August 10, 2022
Sports

Picha 19: Uzinduzi wa Jezi mpya za Simba SC, Mashabiki wafurika Dukani DSM

August 7, 2022
Sports

Simba wafunga usajili kwa kishindo, washusha mshambuliaji kutoka Ulaya

August 7, 2022
Sports

Manara amuingiza Hersi kwenye 18 za TFF

August 7, 2022
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?