Mshambulizi huyo alijiunga na Getafe kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Man United siku ya Makataa huku kinda huyo akitarajia kujenga upya soka lake mbali na umaarufu wa Uingereza kufuatia kukamatwa kwake 2022.
Mwanasoka huyo mwenye utata amekaribishwa kwa mikono miwili katika klabu ya La Liga na kufuatia kuanika kwake mbele ya mashabiki kwenye uwanja wa Coliseum mjini Madrid, Greenwood sasa ameuza jezi nyingi za Getafe zenye jina lake mgongoni ndani ya wiki moja kuliko mchezaji yeyote historia ya klabu\.
Getafe wameuza jezi nyingi zenye jina la Mason Greenwood mgongoni ndani ya wiki moja kuliko walizouza kwa mchezaji yeyote katika historia ya klabu hiyo.
Usajili wa Greenwood, nyota wa zamani wa Man United, ni dili kubwa kwa klabu ndogo kama Getafe lakini mazingira ambayo mwanasoka huyo anasherehekewa yanaacha ladha mbaya mdomoni.
Miamba hao wa Ligi Kuu ya Uingereza waliamua kuachana na kinda huyo mwenye umri wa miaka 21 kutokana na utata wa kukamatwa kwake mwaka 2022, licha ya kufutiwa mashtaka yote mwaka huu. Walakini, ushahidi wa uhalifu wake unaweza kupatikana kwa urahisi na hiyo itamfuata kijana huyo katika maisha yake yote ya uchezaji.