Premier Bet SwahiliFlix Ad Halotel Ad

Habari za Mastaa

Nimekusogezea vitu tofauti usivyovijua kuhusu mastaa hawa 10 na PICHAZ zao!

on

BRIT

Kuna mastaa wengi duniani tunaowajua na kuwapenda sana, na kuna wengine tunatamani kuja kuwa kama wao. Lakini sio kila kitu kuhusu mastaa hawa tunavijua, wengi tunawapenda lakini kuna vitu flani kuhusu wao hatuvijui.

Nimekusogezea picha kumi za mastaa kutoka Marekani, kila mmoja ana kitu chake ambacho labda umewahi au hujawahi kukisikia.
harpo

Television superstaa na millionea Oprah Winfrey wengi tunamfahamu kupitia kipindi chake Oprah Winfrey Show. Lakini maisha yake hayakuwa ya furaha na amani akiwa mtoto, akiwa na miaka 9 aliteswa na ndugu zake na alipokuwa na miaka 14 alibakwa na kupewa mimba na binamu yake, mtoto wake alikufa alipojifungua.

LONDON, UNITED KINGDOM - JULY 13: Jay-Z performs on day 2 of the Yahoo! Wireless Festival at Queen Elizabeth Olympic Park on July 13, 2013 in London, England. (Photo by Joseph Okpako/Getty Images)

Rappa maarufu duniani Jay Z ni miongoni mwa mamilionea wakubwa kwenye Industry ya muziki wa Hip Hop. Lakini na yeye hakuwa na maisha mazuri kwani utotoni aliishi maisha duni sana jijini Brooklyn na alishawahi kumpiga kaka yake risasi akiwa anajaribu kumuibia hela.

lil-wayne

Rappa Lil Wayne ni miongoni mwa marappa wakubwa pia duniani, akiwa chini ya lebo ya Cash Money Records Lil Wayne anafahamika kwa ngoma nyingi kali lakini rappa huyu ana watoto wanne na wanawake wanne tofauti, amabao hajafunga nao ndoa.

busta buss

Busta Rhymes ni msanii mwingine maarufu wa Hip Hop anaejulikana kwa kwa style yake tofauti ya kuimba. Busta Rhymes na rappa Jay Z walisoma shule moja na kupanda basi moja la shule.

minajesty

Nicki Minaj ni rappa mkubwa alianza kutengeneza headlines kubwa miaka ya 2008-2009 kwenye entertainmnet industry na yupo chini na ya Cash Money Records. Lakini Nicki Minaj ana ugonjwa unaoitwa Acrophobic, ugonjwa wa uwoga wa kupanda majengo marefu.

jlo

RnB pop queen Jenifer Lopez ni miongoni mwa wasanii wakubwa katika industry ya muziki duniani, akiwa na zaidi ya rekodi millioni 50. Na katika historia ya wanamziki JLo ana historia ya kuwa na movie na wimbo zilizoshika namba moja kwenye wiki moja.

BRIT

Leona Lewis, Jessie J na Adele ni wasanii kutoka Uingereza walioweza kupenya na kutikisa soko la muziki Marekani na kupata mamilioni ya pesa kupitia nyimbo zao. Kizuri zaidi ni kwamba wasanii hawa watatu walisoma shule moja,The BRIT School of Performing Arts and Technology mwaka 2006 Croydon nchini Uingereza.

Gwen Stefani arrives at the Los Angeles Premiere of Paddington at the TCL Chinese Theatre on Saturday, Jan 10, 2015, in Los Angeles. (Photo by Rob Latour/Invision/AP)

Gwen Stefani ameshinda idadi ya tuzo za Grammy sawa na wasanii Nas, 50 Cent, Busta Ryhmes na Drake.

P-Diddy

Kabla ya kuanza kuimba rasmi, msanii maarufu wa Hip Hop P Diddy alikuwa back-up dancer wa Big Daddy Kane na Heavy D.

madonna

Baada ya kufanya maamuzi ya kufanya muziki msanii wa Pop Marekani Madonna alihamia jijini New York kutimiza ndoto zake, lakini mambo hayakwenda kama anavyotarajia, alijikuta anafanya kazi ya uhudumu kwenye restaurant mbali mbali jijini hapo.

 Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments