Michezo

Kauli ya Juan Mata kuhusu tetesi za Zlatan Ibrahimovic kujiunga Man United

on

March 23 headlines za nahodha wa timu ya taifa ya Sweden anayeichezea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic, jina lake limerudi kwenye headlines baada ya kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea klabu ya Man United Juan Mata kuzungumzia ujio wake Man United.

Juan Mata amezungumzia kuhusu tetesi za muda mrefu kuwa Zlatan atajiunga na Man United mwishoni mwa msimu huu akitokea Paris Saint Germain, Mata ameongea maneno haya baada ya kusikia tetesi hizo.

all-of-zlatan-ibrahimovics-26-league-goals-for-psg-this-season-video

Zlatan Ibrahimovic

“Zlatan ni mchezaji mzuri na siku zote nimekuwa nikipenda kucheza na wachezaji wazuri, sina mamlaka ya kuamua ajiunge na Man United au vinginevyo, nafikiri huo ni uamuzi wake na klabu, kwangu itakuwa faraja kucheza nae ila sijui kama yeye ataamua kujiunga na Man United au kuendelea na PSG” >>> Mata

Bado haijajulikana kama Zlatan atajiunga na Man United mwishoni mwa msimu ila amekuwa akihusishwa kujiunga na vilabu kadhaa ikiwemo Arsenal, Chelsea na Man United. Kwa sasa Zlatan anatajwa kukaribia kumaliza mkataba wake na PSG.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments