Michezo

Matokeo ya Man UTD vs Newcastle – Chelsea vs Stoke City haya hapa

on

HazardRooneyVilabu vya Manchster United na Chelsea leo vimepata ushindi mnono katika mfululizo wa ligi kuu ya Uingereza.

Manchester United ikicheza ugenini katika dimba la St. James Park dhidi ya wenyeji Newcastle imeweza kuifunga timu hiyo magoli 4-0.

Magoli ya Manchester United yalifungwa na Juan Mata aliyefunga mawili, Januzaj na Chicharito nao walifunga kila mmoja goli moja.

Chelsea nao walirudi katika hali ya ushindi baada ya kufungwa wiki iliyopita, leo hii wakicheza nyumbani dhidi ya Stoke City wameweza kutoka na ushindi wa 3-0.

Mohamed Salah, Frank na Willian walifunga magoli ya Chelsea leo hii.

Matokeo mengine Manchester City iliifunga Southmpton 4-0 mapema leo hii.

Tupia Comments