Baada ya kukosa michuano ya ulaya kwa msimu uliopita, hatimaye usiku wa leo Manchester United imerejea rasmi katika michuano hii mikubwa barani humo kwa ngazi ya vilabu.
Vijana wa Louis Van Gaal walisafiri mpaka Uholanzi, nyumbani kwa kocha wao, kucheza na klabu ya PSV.
Mchezo hup umemalizika kwa Manchester kupata mapigo mawili kutoka kwenye mechi hiyo, baada ya kukubali kipigo cha 2-1 na pigp lingine ikiwa ni kuumia vibaya kwa mchezaji wao tegemeo Luke Shaw.
Manchester United walianza kuliona lango la PSV katika dakika ya 41, goli likifungwa na kijana aliyenunuliwa kutoka PSV – Memphis Depay, lakini sekunde kadhaa kabla ya mchezo kwenda mapumziko PSV wakasawazisha kupitia kwa Moreno.
Kipindi cha Narsingh aliifungia PSV goli la ushindi katika dakika ya 57.