Michezo

Matokeo ya mechi za Arsenal vs Hull na Man United vs Everton haya hapa

on

article-2608808-1D396DE700000578-653_964x386Manchester United leo imepoteza mchezo wa 11 wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu.

Timu hiyo inayofundishwa na David Moyes imefungwa kwa mara ya pili na Everton dani ya msimu mmoja baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-0 kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Goodson Park.

Mabao ya Everton yalifungwa na Leighton Baines kwa mkwaju wa penati na Kevin Millaras – magoli yote yalifungwa kwenye kipindi cha kwanza.

Kwa upande wa Arsenal nao wamezidi kuongeza mbio katika kugombania nafasi ya nne mbele ya Everton. Wakicheza kwenye uwanja wao wa nyumbani Hull City walikubali kipigo cha magoli 3-0 kutoka washika bunduki wa Londo. Magoli ya Arsenal yalifungwa na Aaron Ramsey kipindi cha kwanza, kabla ya Podolski kumaliza kazi kwa kufunga bao la 2 na la tatu.

Tupia Comments