Michezo

Matokeo ya Simba vs Prisons – JKT vs Mtibwa Sugar haya hapa

on

DSC_0707Simba ya Dar es Salaam leo imeendelea kuwa na matokeo mabaya kwenye ligi baada ya kushinda kufungana na Prisons ya Mbeya katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Matokeo hayo yanaifanya Simba SC kufikisha 36 baada ya kucheza mechi 21, ikiendelea kubaki nafasi ya nne, wakati Prisons imetimiza pointi 22 baada ya mechi 20 na inabaki nafasi ya 10.

Simba SC leo iliwakilishwa na; Yaw Berko, Haruna Shamte, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haroun Chanongo/Betram Mombeki dk46, Henry Joseph/Said Ndemla dk82, Amri Kiemba, Amisi Tambwe na Ramadhani Singano ‘Messi’/Ali Badru dk70.
Prisons; Beno Kakulanya, Salum Kimenya, Laurian Mpalile, Jumanne Fadhil, Lugano Mwangama, Nurdin Issa, Freddy Chudu, Omega Seme/Jimmy Shoji dk88, Peter Michael/Brighton Mponzi dk86, Frank Hau na Sixbert Mwasekaga.

Wakati huo huo Mtibwa Sugar nao wameangukia pua baada ya kukubali kufungwa 2-1 na JKT Ruvu katika mchezo uliopigwa Chamazi Complex, Mbagala.

Tupia Comments