Michezo

Matokeo ya Yanga Vs JKT Ruvu na mechi zingine za Ligi Kuu yapo hapa (+Pichaz)

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena September 19 kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali Tanzania, mechi ambazo zimechezwa September 19 ni mechi nne, klabu ya Yanga imeikaribisha klabu ya JKT Ruvu ya Pwani katika uwanja wa taifa Dar Es Salaam, huku Stand United ya Shinyanga ikiwa mwenyeji wa African Sports ya Tanga.

DSC_0105

Mgambo Shooting imeikaribisha Maji Maji FC ya Songea katika uwanja wa Mkwakwani Tanga huku uwanja wa Sokoine Mbeya ukipigwa mchezo wa timu zote za jiji hilo Tanzania Prisons dhidi ya Mbeya City.

DSC_0084

Wachezaji wa Yanga wakipongezana baada ya Tambwe kufunga goli

Mechi ya Yanga na JKT Ruvu imemalizika kwa klabu ya Dar Es Salaam Young Africa kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 4-1, magoli ya Yanga yalifungwa na Donald Ngoma dakika 33, Amissi Tambwe dakika ya 48 na 50 huku Thabani Kamusoko akipachika goli la nne dakika 87.

DSC_0025

Simon Msuva akimpiga chenga beki wa JKT Ruvu

3

Haruna Niyonzima katika harakati za kutuliza mpira

DSC_0079

Mbuyu Twite akipatiwa matibabu baada ya kugongana kichwani na mchezaji wa JKT

Matokeo ya mechi zingine zilizopigwa September 19

Stand United 2-0 African Sports

Mgambo Shooting 1-0 Maji Maji FC 

Tanzania Prisons 1-0  Mbeya City

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments