Michezo

Full Time: Simba vs Kagera Sugar na mechi nyingine za bongo Sept. 20

on

Simba SC September 20 imerejea katika uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kumkaribisha mgeni Kagera Sugar huku nahodha wake Mussa Hassan Mgosi akiwa jukwaani, Simba ambayo hadi sasa imecheza mechi mbili na kushinda zote…. kwenye game ya September 20 vs Kagera Sugar, Simba imechukua ushindi wa 3-1.

DSC_0148

DSC_0148

Hamisi Kiiza akishangilia goli lake kwa kusali

Magoli ya Simba yalifungwa kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Hamisi Kiiza dakika ya 30 baada ya kutumia vizuri krosi kutoka kwa Awadhi Juma, Kiiza alipachika magoli mengine mawili dakika ya 46 na 92 huku Kagera Sugar wakiambulia goli moja lililofungwa na Mubaraka Yusuph dakika ya 60.

DSC_0129

Nahodha wa Kagera Sugar George Kavilla akiwania mpira na Peter Mwalyanza

DSC_0123

Hamisi Kiiza akidhibitiwa maridadi na mchezaji wa Kagera Sugar

DSC_0109

Ibrahim Ajib akimpiga chenga beki wa Kagera Sugar

DSC_0106

Simon Sserunkuma akidhibitiwa na beki wa Kagera Sugar

DSC_0049

Salum Kanoni akimdhibiti Ibrahim Ajib

DSC_0117

Hassan Kessy wa Simba akimdhibiti beki mwenzie wa Kagera Sugar asipite

DSC_0074

Wachezaji wa Simba wakishangilia kwa pamoja goli la tatu la Kiiza

Haya ni matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa September 20

Mwadui FC 0 – 1 Azam FC

Mtibwa Sugar 2 – 1 Ndanda FC

Coastal Union 0 – 0 Toto Africans

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments