Michezo

Unayataka matokeo ya Mbeya City vs Yanga leo, ya Azam je?

By

on

yangaaaKutoka uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam mechi kati ya Yanga na Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania, Yanga imechukua ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City kutoka 87.8 Mbeya.

Kwa sasa Yanga inabaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu baada ya Azam FC leo kuifunga Kagera Sugar 4-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es Salaam ambapo kwa sasa Azam FC ina jumla ya pointi 36 na Yanga 35 baada ya kila timu kucheza mechi 16.

Bao la Yanga lilifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 16 baada ya kuuwahi mpira uliorudishwa na mabeki wa Mbeya City  dakika ya pili baada ya mpira kuanza ambapo kwenye kipindi cha pili Mbeya City walipata pigo baada ya kiungo wao Steven Mazanda kupewa kadi nyekundu.

Upande wa Uwanja wa Azam Complex magoli ya Azam, mawili yalifungwa na Brian Umony dakika za 13 na 48, Kevin Friday dakika ya 51 na Jabir Aziz dakika ya 83.

Tupia Comments