Top Stories

Baada ya matokeo kuanza kutangazwa, CCM kaongea January.. UKAWA kaongea Lowassa

on

Ni saa chache zimepita toka zoezi la kupiga kura kukamilika katika maeneo mbalimbali Tanzania na sasa vichwa vya habari vikihamia kwenye matokeo na utangazwaji wake ambapo wakati matokeo ya kura za Urais yakianza kutangazwa October 26, vyama vya siasa CCM na UKAWA vimeyasema yafuatayo mbele ya Waandishi wa habari.

Hapa naanza na Edward Lowassa ambaye ni mgombea Urais kwa ticket ya UKAWA.

Nimewaita kueleza masikitiko mawili… kwanza upande wa jeshi la Polisi… tuna vijana wetu wanaofanya kazi za IT kwa kujitolea maeneo ya Kinondoni na Kijitonyama jumla ya vituo vitatu hawa vijana wanafanya uzalendo kushiriki katika uchaguzi wa nchi yao na kujenga historia mpya ya nchi yao, tendo la kuwakamata si la haki kabisa.” >>> Edward Lowassa.

Lowassa-2

“Jana Polisi wamevamia maeneo yao waliyokua wanafanyia kazi Kinondoni maeneo mawili na Kijitonyama eneo moja, wamewakamata na vifaa vyao na kuwafunga, kinachosikitisha zaidi ni tuhuma wanazowatuhumu za usafirishaji wa binaadamu… kosa ambalo ni kubwa sana kisheria na halihusiani na walichokua wanafanya, tumeeleza masikitiko yetu kwa Polisi kuchukua hatua wakati huu tunapohitaji vijana hawa, wanafanya kazi ya hesabu ya kura zinakwendaje’ – Edward Lowassa

‘Mpaka sasa hivi wako wameshikwa, nimempigia Mkuu wa Polisi Tanzania na kumwelezea……. kingine cha pili nimeona tangazo lao la kura lakini nikadhani linaweza kuboreshwa, linaelekea upande ule unaopendelea Magufuli zaidi, tungetaka tu wachukue zile kura wahesabu zote kwa pamoja sio wachukue mbili zinazompendelea ionekane wanawaandaa watu kisaikolojia kwamba ana ushindi, watangaze kwa namna ambayo haina upendeleo’ – Edward Lowassa.

3X6A9467

HAPA CHINI NI TAARIFA ILIYOTOLEWA NA CCM KUPITIA KWA JANUARY MAKAMBA

Kuhusu upigaji wa Kura: “CCM inahimiza utulivu kwa wananchi na kuziachia mamlaka husika zifanye kazi yake… kazi za vyama ni kupokea matokeo na kazi ya Tume ni kuyatangaza, tunasikitishwa na propaganda zinazoendeshwa kuhusu matokeo ya uchaguzi… tunaona matokeo yanayotangazwa na wafuasi wa vyama vya upinzani hasa mitandaoni… matokeo rasmi yatatolewa na tume, bahati mbaya sana wengine wanatoa matokeo ya uongo mapema ili tume ikitoa matokeo rasmi waseme wameibiwa” >>> January Makamba.

Screen Shot 2015-10-26 at 7.17.05 PM

‘Sisi kama CCM tumeridhishwa na amani na utulivu uliotawala katika sehemu kubwa ya nchi yetu wakati wa kupiga kura jana, licha ya changamoto zilizojitokeza ambazo baadhi zimeshughulikiwa na tume, jinsi zoezi la kupiga kura linavyoendeshwa sasa kwa uwazi… matokeo ya uchaguzi huu yatakua kielelezo halisi cha utashi wa Watanzania kuhusu viongozi wanaowataka hivyo hakuna sababu yoyote ya kuyakataa matokeo’ – January Makamba

Mkakati wa wapinzani kuitaka Jumuiya ya kimataifa itumie nguvu yake ya misaada kwa nchi yetu kulazimisha matokeo ambayo hayatokani na utashi wa watanzania, CCM haitalikubali jambo hili, tumeona wameajiri kabisa Magwiji wa Propaganda wa kimataifa kwa fedha nyingi ili wawasaidie kujenga taswira duniani kwamba Tanzania ni sawa na nchi nyingine ya Afrika inatawaliwa ovyo inataka kuiba uchaguzi’January Makamba

Kwenye sentensi nyingine, January Makamba amesema >>> ‘Sasa mkakati wao ni kuishinikisha kuilazimisha jumuiya ya kimataifa itangaze mgogoro wa kisiasa Tanzania kwa kutumia nguvu ya misaada yake na kulazimisha matokeo au mkao mpya wa siasa ambao hautokani kabisa na utashi wa wapiga kura

Screen Shot 2015-10-26 at 7.17.14 PM

Kwa kumalizia January Makamba amesema >>> ‘Sisi hatuna mamlaka ya kutangaza matokeo kisheria lakini kwa upande mwingine matokeo haya yanabandikwa na Wasimamizi wa vituo kwenye vituo vya kupiga kura kwahiyo ni matokeo ambayo yako hadharani, na kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyoko hadharani, CCM tumeona katika majimbo 264 Tanzania hadi sasa tumeshachukua majimbo 176 na kukomboa Majimbo 12 yaliyokua yanashikiliwa na Upinzani, tunaomba WanaCCM watulie tume imalize kazi yake

Hapa chini kuna sauti za January Makamba na Edward Lowassa wakiongea kuhusu hizi taarifa za leo.

Sauti ya Edward Lowassa hii hapa pia.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andikaAYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments