Matumizi mabaya ya mtandaoni ni tishio la moja kwa moja kwa uhuru wa kujieleza na yanaweza kuwa na athari mbaya kwa tija yako, hali nzuri ya mwili na afya ya akili.
Lakini kupitia elimu ya usalama mtandao inasaidia kupunguza athari za uhalifu mtandao ambazo husababishwa na udhaifu wa mwanadamu.
Hivyo, programu ya elimu kwa umma ya matumizi salama ya mtandao ni dhana muhimu inayoongeza ujuzi na maarifa kwa watendaji na kuwawezesha kubaini viashiria vya mashambulizi kabla ya kusababisha madhara kwa mwananchi, taasisi na nchi kwa ujumla.
Elimu kwa umma ya usalama mtandao ya mara kwa mara ni muhimu kwa biashara na taasisi hususan kwa kuwa inazuia changamoto kadhaa kama vile kupigwa faini kwa mujibu wa sheria, upotevu wa fedha, upotevu wa haki miliki, uharibifu wa taswira ya taasisi/biashara, upotevu wa wateja, n.k.
Kupitia elimu hii yapo mambo kadhaa ya kujihadharisha utumiapo ama unapoanza kutumia mitandao ya kijamii
1. Jiridhishe kabla ya kufungua au kupakua chochote mtandaoni
Ikitokea umepokea barua pepe inayoonekana imetoka kwa mtu unayemfahamu, kuwa makini kabla ya kufungua viambatisho vyake. Ni vema ukiwa na mashaka uchukue tahadhari au kutojibu barua pepe husika kwa sababu utambulisho wa mhusika unaweza kuwa umedukuliwa.
2. Tumia programu za kujilinda mtandaoni
Programu ya kulinda vifaa vya TEHAMA (AV) imekuwa suluhisho zuri la kupambana na mashambulizi ya virusi mtandaoni. Programu ya AV huzuia virusi vya mtandao kuingia kwenye kifaa chako na kuhatarisha usalama wa taarifa. Inashauriwa kutumia programu moja ya kuzuia virusi mtandaoni kutoka kwa wachuuzi wanaoaminika.
3. Jiridhishe maombi ya taarifa binafsi
Unapoombwa kutoa taarifa zako binafsi au za mtu mwingine, hakikisha unajiridhisha na utambulisho wa mwombaji – hata kama inaonekana kuwa ni mtu unayemfahamu. Matapeli wana mbinu nyingi za kukusanya, kuiba taarifa au utambulisho wa mtu ili kuzitumia kufanya uhalifu. Jenga tabia ya kuangalia mara kwa mara taarifa zako za kifedha.
4. Linda nywila zako
Usitoe nywila au nambari ya siri (PIN) kwa mtu yeyote. Hakikisha nywila ni ndefu, imara na ya kipekee. inashauriwa utumie uthibitishaji wa vipengele vingi kadiri ya inavyowezekana (mfano alama za vidole, kadi, jumbe za uthibitisho kwa namba binafsi za simu au barua pepe, n.k.).
5.Tumia nywila/nambari ya siri tofauti kwa akaunti tofauti au tumia nywila/nambari ya siri tofauti kazini na nyumbani; na
Usikubali programu na tovuti kukumbuka nywila zako.
5. Matumizi salama ya vifaa vya TEHAMA vya mkononi
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kampuni ya McAfee Labs ya Marekani, matukio mapya milioni 1.5 ya programu hasidi na virusi mtandaoni yanalenga zaidi vifaa vya TEHAMA vya mkononi.
Dondoo muhimu za usalama wa vifaa vya TEHAMA vya mkononi:
Tengeneza Nambari ya siri (PIN) yakipekee.
Inashauriwa kutotumia tarehe ya kuzaliwa au namba ya simu;
Sakinisha (Install) programu tumizi (Application) kutoka kwenye vyanzo vinavyoaminika;
Hakikisha kifaa chako kimesasishwa (updated) – Wadukuzi hutumia udhaifu uliopo katika programu au mifumo ambayo haijasasishwa kuingilia vifaa au