Habari za Mastaa

Baada ya miaka 22 Notorious apewa heshima na mji wa New York (+Video)

on

Kupitia mahojiano na kipindi cha radio cha Hot 97 mama mzazi wa marehemu Notorious B.I.G ambaye ni Ms. Voletta ameweka wazi kuwa mji wa New York umeamua kumpa heshima mwanae kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwenye game ya muziki wa Hip Hop pamoja na mtaa aliokuwa anaishi.

Notorious B.I.G ambaye alifariki miaka 22 iliyopita amepewa moja ya mtaa na kuitwa jina lake, Ms. Voletta ameeleza kuwa mtaa huo utaitwa ‘Christopher Wallace Way’ na umezinduliwa rasmi June 10,2019 katika makutano ya barabara ya St James Place na mtaa wa Fulton Brooklyn Marekani.

Enzi za uhai wake Notorious akiwa na P Diddy

“Hatimaye kutakua na mtaa utakaoitwa Christopher Wallace Way, kuna vitu vingi vilisemwa lakini inakubidi ufanye kazi kwa bidii nakumbuka mwaka 1997 baada ya kifo cha Christopher Mwanasheria alishauri hiki kitu lakini sikupendezwa nacho kwa sababu nilikua bado kwenye majonzi, sikutaka kuona jina lake popote ingeniumiza zaidi” >>> alisema mama mzazi wa Notorious.

Notorious B.I.G ambaye jina lake halisi ni Christopher Wallace alizaliwa  May 21, 1972 New York Marekani na kufariki March 9 1997 kwa kupigwa risasi na enzi za uhai wake aliacha ngoma kibao ikiwemo One more chance, Dead Wrong, Juicy, Who shot Ya na nyingine nyingi.

VIDEO: CHUCHU HANS MBELE YA WAANDISHI WA HABARI KATAJA SIFA NA VIGEZO VYA KUSHIRIKI MISS TANGA

Soma na hizi

Tupia Comments