Top Stories

MAUAJI SINZA: Alimmiminia risasi kama mbuzi, muuaji alivurugwa na shetani (+video)

on

Wengi wetu tumeona video na picha zilizosambaa za tukio la Mtu kupigwa risasi akiwa Baa Sinza kwa Remi Dar es salaam usiku wa July 17 2021.

Kwa mujibu wa shuhuda ambae pia ni Rafiki, Kijana aliyepigwa risasi na kufariki anaitwa Gift na alikua amekaa jirani na Alex na alisimama kumtuliza Alex baada ya kuona ameanza kutishia Watu kwa bastola yake, amesema Shuhuda huyu.

“Gift ni Kijana mwenzangu tukifanya kazi Ofisi moja, alikua ana muomba Alex asipige risasi kama vile na kupoteza amani, yani kitendo cha Gift kumsemesha yule Jamaa imekua kama kosa aligeuka akammiminia Gift risasi nyingi kama mbuzi, Gift kuona vile akakimbia lakini akaishiwa nguvu hatua chache tu”

“Tulishindwa kutoa msaada kwa Gift kwasababu Jamaa mwenye Bastola (Alex) alikua kama amevurugwa Shetani kama amemuingia anageuka anaangalia nani mwingine ampige risasi…………..”

Soma na hizi

Tupia Comments