AyoTV

VIDEO: Waziri Maghembe kuhusu kuuawa kwa aliyefanikisha kukamatwa “malkia wa pembe za ndovu”

on

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe  amekutana na waandishi wa habari kueleza kuhusu wahalifu ambao wamekamatwa na meno ya Tembo.

Wakati akifafanua kuhusu kukamatwa kwa wahalifu hao na meno ya Tembo, Waziri Magembe ameeleza kuhusu Mpelelezi kinara aliyefanikisha kukamatwa kwa Yang Feng Glan maarufu kama ‘Malkia wa Meno ya Tembo’Wayne Lotter kuuawa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Waziri Maghembe amesema alikuwa Lotter alikuwa ni mshirika mkubwa katika kupambana na ujangili lakini ameomba watu kuwa na subira wakati huu jeshi la polisi likiendelea na upelelezi.

Wayne Lotter, 51, alipigwa risasi Jumatano jioni katika maeneo ya Masaki, Dar es Salaam wakati akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo taxi alilopanda lilisimamishwa na gari lingine kabla ya watu wawili kutelemka na kumpiga risasi. Bonyeza play hapa chini kuitazama

VIDEO: Masharti ambayo raia wa Afrika Kusini ameambiwa ili apate dhamana, Bonyeza play hapa chini kutazama 

Soma na hizi

Tupia Comments