Habari za Mastaa

Rich Mavoko ameeleza sababu ya kumpa mtoto wake jina la baba yake Dokii

on

Staa wa Bongofleva kutoka WCB, Rich Mavoko ambaye anatamba na wimbo wa ‘Show Me’ alioimba na Harmonize kutoka WCB pia amesema amempa mtoto wake jina la baba yake Dokii kwa kuwa yeye na Dokii ni ndugu.

Kupitia XXL ya Clouds FM leo April 19, 2017 Mavoko amesema hayo baada ya kuulizwa kuhusu jina la mtoto wake na kusema:>>>“Mwanangu anaitwa Wency, ni jina la baba yake Dokii. Mimi na Dokii ni ndugu.” – Rich Mavoko.

Pamoja na hilo, Mavoko amezungumzia kuhusu kubadili style ya nywele pamoja na tuzo ya jiwe la mwezi ambapo akisema: >>>”Nimeamua mwenyewe nibadilishe muonekano wangu wa nywele. Kuhusu cheti nilichopata kwenye Jiwe La Mwezi, kwangu ni kitu kikubwa sana na asanteni kwa kutupa thamani wasanii.” – Rich Mavoko.

VIDEO: Harmonize na Rich Mavoko walivyoitambulisha ‘Show Me’ Mbagala

Soma na hizi

Tupia Comments