Serikali kupitia wizara ya kilimo imeandaa maeneo wezeshi ya kilimo kwa vijana ili kuwekeza kwenye kilimo na kuwaondoa kwenye maisha ya kubet.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde katika mkutano wa wahariri na wandishi wa habari jijini Dodoma uliolenga kutekeleza ushiriki wa vijana katika kilimo biashara programu inayotarajia kuongeza ajira kwa vijana 3000 na kuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo hadi kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2030
“Vijana wetu wanatamani kufanya kilimo lakini miundombinu yakuwafanya wakafanya kilimo haikuwa rafiki sana sisi tumeamua wizara ya kilimo tumeamua kukifanya kilimo kiwe sex kivutie na vijana watoke kwenye kubet wakalime kwahiyo tulichokiamua tuliweka mazingira rafiki kumfanya kijana avutike akalime tumeamua kusafisha maeneo na kuweka miundombinu,tutawasaidia miundombinu na tutaqatafutia masoko” Anthony Mavunde